Maelezo ya Chini
a “Nyakati za kurudishwa kwa mambo yote” zilianza wakati Ufalme wa Kimesiya uliposimamishwa, mrithi wa Mfalme Daudi aliyekuwa mwaminifu alipowekwa kuwa mtawala wa Ufalme huo. Yehova alikuwa amemwahidi Daudi kwamba mrithi wake angetawala milele. (Zaburi 89:35-37) Lakini baada ya Babiloni kuharibu Yerusalemu mnamo mwaka wa 607 K.W.K., kiti cha enzi cha Mungu hakikukaliwa na mwanadamu mwingine yeyote aliye mzao wa Daudi. Yesu, aliyezaliwa duniani akiwa mrithi wa Daudi, akawa Mfalme aliyeahidiwa tangu kale alipotawazwa mbinguni.