Maelezo ya Chini
a Bahari ya Galilaya hupata dhoruba za ghafula mara nyingi. Kwa sababu bahari hiyo iko chini sana (meta 200 chini ya usawa wa bahari), eneo hilo lina joto kuliko maeneo ya karibu, kwa hiyo, hali ya hewa hubadilika ghafula. Pepo kali sana huvuma kwenye Bonde la Yordani kutoka kwenye Mlima Hermoni ulio upande wa kaskazini. Dhoruba kali inaweza kutokea ghafula na kuvuruga bahari.