Maelezo ya Chini
c Kutema mate kulikuwa njia au ishara ya kuponya iliyokubaliwa na Wayahudi na Wasio Wayahudi. Na maandishi ya marabi yanataja tiba ya kutumia mate. Huenda Yesu alitema mate ili kumjulisha mtu huyo kwamba alitaka kumponya. Vyovyote iwavyo, Yesu hakuwa akitumia mate yake kama dawa ya asili.