Maelezo ya Chini
a Qurani inataja kuzaliwa kwa Yesu kimuujiza kwenye Sura ya 19 (Mariamu). Inasema: “Tukampelekea [Mariamu] Muhuisha Sharia yetu (Jibrili)—akajimithilisha kwake (kwa sura ya) binadamu aliye kamili. (Mariamu) akasema: ‘Hakika mimi najikinga kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema (Aniepushe) nawe. Ikiwa unamuogopa Mungu (basi ondoka nenda zako).’ (Malaika) akasema: ‘Hakika mimi ni Mjumbe wa Mola wako: ili nikupe mwana mtakatifu.’ Akasema: ‘Nitawezaje kupata mtoto, hali hajanigusa mwanamume (yoyote kwa njia halali) wala mimi si (mwanamke) mwenye kuzini.’ (Malaika) akasema: ‘Ni kama hivyo (unavyosema; lakini) Mola wako amesema: “Haya ni sahali Kwangu, na ili Tumfanye Muujiza kwa wanaadamu na rehema itokayo kwetu (ndiyo tumefanya hivi);” na hili ni jambo lililokwisha hukumiwa.’”