Maelezo ya Chini
a Mnamo Novemba 2002, kabla ya vita kuzuka nchini Iraki, Profesa Dan Cruickshank alizuru eneo hilo. Aliripoti hivi kwenye televisheni ya shirika la utangazaji la BBC: ‘Pembeni mwa jiji la Mosul kuna magofu ya jiji kubwa la Ninawi. Kuanzia miaka ya 1840 na kuendelea, waakiolojia wa Uingereza wenye hamu ya uvumbuzi walichimbua magofu ya jiji hilo pamoja na ya jiji la Nimrud. Kutembelea majiji hayo ya Ashuru kuliongoza kwenye uvumbuzi wa ustaarabu wa kale sana. Ustaarabu huo uliokuwa umesahaulika, umetajwa kifupi katika Biblia.’