Maelezo ya Chini
a Baadhi ya wapinzani hao walikuwa sehemu ya “Sinagogi la Watu Waliowekwa Huru.” Huenda walikuwa watu waliokuwa wamekamatwa na Waroma kisha wakaachiliwa, au huenda walikuwa watumwa waliowekwa huru kisha wakawa Wayahudi wageuzwa imani. Baadhi yao walikuwa wenyeji wa Kilikia, alikotoka Sauli wa Tarso. Masimulizi hayo hayataji iwapo Sauli alikuwa miongoni mwa Wakilikia waliokuwa wameshindwa kuthibitisha kwamba walikuwa sahihi kuhusu madai yao dhidi ya Stefano.