Maelezo ya Chini
b Agano la tohara halikuwa sehemu ya agano la Kiabrahamu linalotumika mpaka leo. Agano la Kiabrahamu lilianzishwa mwaka wa 1943 K.W.K., wakati ambapo Abrahamu (aliyekuwa akiitwa Abramu), alivuka Mto Efrati akielekea Kanaani. Alikuwa na umri wa miaka 75. Agano la tohara lilianzishwa baadaye, mwaka wa 1919 K.W.K., Abrahamu alipokuwa na umri wa miaka 99.—Mwa. 12:1-8; 17:1, 9-14; Gal. 3:17.