c Inaonekana kwamba Tito, Mkristo Mgiriki ambaye baadaye alifanya kazi bega kwa bega na Paulo, alikuwa miongoni mwa wale waliotumwa Yerusalemu. (Gal. 2:1; Tito 1:4) Alikuwa Mtu wa Mataifa asiyetahiriwa, lakini alitiwa mafuta kwa roho takatifu na alikuwa ndugu mwenye mfano mzuri.—Gal. 2:3.