Maelezo ya Chini
a Andiko la Mwanzo 2:10-14 husema: “Kulikuwa na mto unaotoka katika Edeni ili kuinywesha bustani maji, na kutoka hapo ukaanza kugawanyika na kuwa vichwa vinne. Jina la ule wa kwanza ni Pishoni . . . jina la mto wa pili ni Gihoni . . . jina la mto wa tatu ni Hidekeli [au, Tigri]; ndio unaoelekea upande wa mashariki wa Ashuru. Na mto wa nne ni Efrati.” Mito miwili ya kwanza haijulikani wala mahali ilipokuwa hapajulikani.