Maelezo ya Chini
a Kitabu Molecular Biology of the Cell hutumia kipimo tofauti. Kinasema kwamba kujaribu kupanga nyuzi hizo ndefu ndani ya kiini cha chembe ni kama kujaribu kupanga uzi mwembamba sana wenye urefu wa kilomita 40 ndani ya mpira wa tenisi—lakini kwa utaratibu mzuri hivi kwamba kila sehemu ya uzi huo inaweza kufikiwa kwa urahisi.