Maelezo ya Chini
a Kama Naomi alivyosema, Yehova hawaonyeshi tu fadhili walio hai; bali pia wafu. Naomi alikuwa amefiwa na mumewe na wanawe wawili. Naye Ruthu alikuwa amefiwa na mumewe. Bila shaka, wanaume hao watatu walipendwa sana na wanawake hawa wawili. Fadhili zozote ambazo Ruthu na Naomi walionyeshwa, zilikuwa fadhili kuelekea wanaume hao ambao wangetaka wanawake hawa wapendwa watunzwe.