Maelezo ya Chini
a Mfano wa Yesu huenda uliwakumbusha wasikilizaji wake kuhusu Arkelao, mwana wa Herode Mkuu. Kabla ya Herode kufa, alimchagua Arkelao arithi utawala wa Yudea na maeneo mengine. Hata hivyo, kabla ya kuanza kutawala, ilibidi Arkelao asafiri safari ndefu hadi Roma ili kupata kibali cha Kaisari Augusto.