Maelezo ya Chini
a Wayahudi wengi wahamishwa waliishi katika vijiji vilivyokuwa mbali na jiji la Babiloni. Kwa mfano, Ezekieli aliishi kati ya Wayahudi walioishi kando ya mto Kebari. (Eze. 3:15) Hata hivyo, kuna wahamishwa wachache Wayahudi walioishi jijini. Walitia ndani wale waliotoka katika “uzao wa kifalme na wa watu mashuhuri.”—Dan. 1:3, 6; 2 Fal. 24:15.