Maelezo ya Chini
a Isitoshe, Wayahudi wahamishwa ambao walikumbuka mandhari ya kijiografia ya nchi yao inaelekea walijua kwamba mto huo haukuwa halisi kwa sababu ulitiririka kutoka hekaluni kwenye mlima mrefu sana, ambao kihalisi haukuwepo katika eneo lililotajwa. Pia, maono hayo yalidokeza kwamba mto huo ulitiririka moja kwa moja hadi kwenye Bahari ya Chumvi, jambo ambalo halingewezekana kulingana na mandhari ya kijiografia ya eneo hilo.