Maelezo ya Chini
a Nyakati nyingine matibabu ya ugonjwa, kama cancer ya shingo huua kijitoto kilichoanza kuumbika ndani ya mimba. Lakini huenda jambo hilo lisiepukike: kuharibu mimba siyo matibabu ya ugonjwa huo wala hakufanywi kwa makusudi. Vivyo hivyo, nyakati nyingine mbegu ya mwanamke iliyotiwa mimba hubaki katika mrija (fallopian tube) unaotumiwa na yai linaposafiri kutoka mfuko wa mayai kuelekea kwenye mji wa mimba, kisha mbegu hiyo huanza kukulia mrijani badala ya kukulia katika mji wa mimba. Mimba hiyo iliyokaa mahali pabaya haiwezi kuwa mtoto katika mrija huo mdogo; baadaye itakwisha na kapasua mrija na kuua kijitoto kilichokuwa kimeanza kuumbika. Kwa kawaida madaktari huponya hali hiyo kwa kuondoa mrija huo kabla haujapasuka, ikiwa wameiona hali hiyo mapema. Mwanamke Mkristo mwenye mimba katika mrija aweza kuamua kama atakubali kupasuliwa. Katika hali za kawaida, bila shaka angekuwa na nia ya kukabili hatari zo zote za mimba ili mtoto wake aweze kuishi. Lakini mimba ikikaa katika mrija anakuwa katika hatari kubwa na hali kijitoto kilichokuwa kimeanza kuumbika hakiwezi kuendelea kuishi na kuzaliwa.