Maelezo ya Chini
a Kitabu cha mkusanyo wa mapokeo ya Kiyahudi kiitwacho Mishinah kinataja wazi namna 39 za kazi kubwa zilizokatazwa katika siku ya sabato, pamoja na kazi nyingine ndogo-ndogo. Kati ya kazi zilizokatazwa ni kupepeta, kupura, kusaga na kupembua. (Kijitabu Shabbath 7:2) Kitabu kiitwacho Palestinian Talmud kinatoa maoni ya marabi juu ya kazi kama hizo zilizokatazwa: ‘Ikiwa mwanamke anajongeza ngano ili ayatoe makumvi, hii inaonwa kuwa ni kupepeta; akisugua masuke ya ngano, inaonwa kuwa ni kupura; akitoa yanayokwama kando-kando, ni kupepeta matunda; akikwarusa masuke, ni kusaga; akiyatupa juu mikononi mwake, ni kupembua.’