Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO

Maelezo ya Chini

b Kitabu The Theological Dictionary of the New Testament chasema hivi juu ya Sanhedrin kuu katika Yerusalemu: “Mbele ya baraza hiyo, iliyokutanika katika boule [chumba cha baraza] . . . kuhani mkuu alisimama. Ndiye aliyekuwa kiongozi cha Wayahudi; yeye peke yake ndiye angeisimamia Sanhedrin. Kumzunguka walikuwako archiereis [wakuu wa makuhani], wakuu wa kikuhani, Masadukayo waliowaunga mkono. Kwa uwezo wa cheo makuhani wakuu hekaluni walikuwa na cheo na mamlaka katika Sanhedrin na walifanyiza chama chenye nguvu nyingi. Wazee walikuwa kikundi cha pili. Ni kweli kwamba hapo kwanza washiriki wote wa gerousia [baraza ya wanaume wazee] waliitwa wazee. Hata hivyo, polepole, neno hilo likawa na maana fulani ya pekee, ikawa kwamba viongozi wa jamaa zenye mamlaka katika Yerusalemu peke yao ndio walioitwa Presbyteroi [wazee]. Vilevile, wakuu hawa wote, walikuwa wa imani ya Masadukayo. Mafarisayo walifaulu kuingia katika Baraza Kuu katika siku za Malkia Aleksandra [76-67 K.W.K.]. Tangu wakati huo uweza na uongozi wa grammateis [waandishi] uliendelea kuwa imara katika Sanhedrin. Wakati wa kipindi cha Warumi archierieis [wakuu wa makuhani] walikuwa wangali na cheo cha kwanza, walakini kwa kweli maamuzi hayangefanywa au kufikilizwa pasipo kibali ya waandishi wa Kifarisayo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki