Maelezo ya Chini
a Kuhusu kusali barabarani na mahali pa watu wote, maandishi ya kirabi ya Wayahudi yanatoa mifano kama huu ufuatao: “Rabi Yokanani amesema: ‘Niliona namna Rabi Yanai alivyokuwa akisimama na kutoa sala ya Musaf [nyongeza]:’ “(Palestinian Talmud) “Ikiwa mtu amesimama akiomba barabarani au mahali palipo wazi, husogea kando [apishe punda], mpanda punda au mbeba mzigo pasipo kukatisha sala yake. Kuhusu Rabi Chanina ben Dosa [wapata mwaka 70 W.K.] inasimuliwa kwamba alikuwa amesimama akiomba. Halafu nyoka mwenye sumu akamwuma. Hata hivyo, yeye, hakukatiza sala yake.”—Tosephta (maandishi ya nyongeza ya Mishnah).