Maelezo ya Chini
a Kwa habari ya Mafarisayo kama manabii wa uongo, David Hill aandika hivi katika gazeti Biblica (1976, Vol. 57); “Josephus awajua Mafarisayo waliokuwa na [uwezo wa kutabiri] matukio ya wakati ujao nao walitumia kipawa chao kuendeleza siasa (Ant. XVII 41-45), na mahali pengine anazungumza juu ya mtu fulani aitwaye Pollion na mwanafunzi wake Samaias waliotabiri (Ant. XIV 172-176; XV 3, 370). Walakini ulio wa maana hata zaidi ya habari ya Josephus iliyo chache na pengine iliyovurugika ni uhakika wa kwamba Mafarisayo kama kikundi walijiona wenyewe kuwa warithi wa mapokeo makubwa ya kiunabii: walirithi mapokeo hayo kutoka kwa wanaume wa ule Mkusanyiko Mkubwa ambao uliyarithi kutoka kwa nabii wa mwisho wa nasaba ya manabii. Wakiwa wafasiri wenye ujuzi wa Maandiko Mafarisayo walitumia njia iliyokaribia sana katika wakati wao ufunuo uliopelekwa kupitia kwa manabii wa wakati wa mapema. . . . Kwa habari yao, na warithi wao, ingeweza kusemwa kwamba ‘Ikiwa wao si manabii, hata hivyo wao ni wana wa manabii’ (ilisemwa juu ya Hillel [rabi aliyeishi karibu na wakati ule ule mmoja na Yesu]). Linalopatana kabisa na hili ni lile neno la Yesu juu ya Mafarisayo wakijenga makaburi ya manabii na kuyapamba maziara ya wenye haki (Mt. 23:29). Kwa hiyo si Jambo lisilowezekana kwamba Mafarisayo katika siku za Yesu walidai kuwa na cheo na mamlaka (ikiwa hawakudai jina) la nabii.”