Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO

Maelezo ya Chini

a Kwa habari ya Wayahudi kutoa pepo, twasoma hivi katika kitabu Exorcism Through the Ages (Kupunga Pepo Wakati wa Vizazi Vyote): “Jambo kubwa la kupunga pepo kwa Kiyahudi ni kupa jina kwa majina yanayoaminika kuwa yanafaa, yaani, majina ya malaika wema, ambayo ama yanatumiwa peke yake au kwa kuunganisha pamoja na El (=Mungu); hakika kutegemea majina tu kulikuwa kumekuwa ushirikina wa Wayahudi zamani sana, na lilionekana kuwa jambo la muhimu sana kwamba majina yanayofaa, ambayo yalitofautiana nyakati na pindi mbalimbali, yatumiwe. Lilikuwa sadikisho hilo la ushirikina, bila shaka, lililowasukuma wana wa Skewa, ambao walikuwa wameshuhudia kupunga pepo kulikofanikiwa kwa Mtakatifu Paulo katika jina la Yesu, wajaribu kwa kujitakia wenyewe njia hiyo, ‘Nawaapisha kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri,’ wakawa na matokeo yenye msiba (Matendo, 19:13). Lilikuwa sadikisho la Kiyahudi lenye kupendwa na watu wengi, lililokubaliwa hata Yosefo mtu asiyependelea taifa lo lote ambaye alikuwa amesoma sana, kwamba Sulemani alikuwa amepata uwezo wa kutoa pepo, na kwamba alikuwa amebuni na kupokezana njia fulani ambazo zililifaa kusudi hilo. Mwanahistoria huyo Myahudi ameandika namna Eleazari fulani, mbele ya Mfalme Vespasian na maafisa (wakuu) wake, alivyofaulu, kwa kutumia pete ya kimwujiza iliyowekwa puani mwa mtu aliyepagawa, kuvuta pepo puani—uwezo huo wa pete ukiwa ni kwa ajili ya uhakika wa kwamba ilikuwa na mzizi fulani usio wa kawaida ndani yake ambao ulionyeshwa katika njia za kutokeza tendo za Sulemani, na ambao ulikuwa haupatikani kwa urahisi hata kidogo.”​—Tazama kitabu Antiquities of the Jews cha Yosefo, Kitabu 8, sura 2, sehemu 5 na kitabu The Jewish War, Kitabu 7, sura 6, sehemu 3.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki