Maelezo ya Chini
c Joseph Bingham mwanahistoria wa kidini aandika hivi juu ya karne za kwanza-kwanza: “Adhabu iliyotolewa na kanisa ilikuwa na uwezo wa kuwanyima watu faida zote na mapendeleo yote yanayotokana na ubatizo, kwa kuwaondoa katika jamii ya kanisa na ushirika walo, . . . na kila mtu aliwaepuka katika mazungumzo yale ya kawaida, kwa upande mmoja akiwa na kusudi la kuwathibitishia mambo ambayo kanisa halikutaka wapate na hatua zilizochukuliwa juu yao, na kwa upande mwingine akiwa na kusudi la kuwaaibisha, na kwa upande mwingine kujipatia usalama kusiwe na hatari ya kuambukizwa na mtu huyo hali yake yenye makosa.” “... hakuna mtu aliyepaswa kuwapokea katika nyumba yake watu waliotengwa na ushirika, wala kula kwenye meza moja pamoja nao; watu hawakupaswa kuzungumza nao kama watu wanaofahamiana, wakiwa wangali hai; wala hawakupaswa kuwafanyia sherehe za maziko, wakati walipokufa, . . . Maagizo hayo yalitolewa kwa kufuatisha kielelezo cha sheria za mitume, zilizowakataza Wakristo wasiwaunge mkono kwa njia yo yote wakosaji wenye sifa mbaya sana.”—Kitabu The Antiquities of the Christian Church (Desturi za Kale za Kanisa la Kikristo), kur. 880, 891.