Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO

Maelezo ya Chini

a Katika nyakati za Biblia, sawa na leo, watu wengine waliweza kusoma na wengine hawakuweza, lakini huenda ikawa kwamba watu wa sehemu nyingi sana waliweza kusoma, wala si kama vile watu wengi wamekuwa wakidhani kwamba wengi hawakujua kusoma siku hizo. (Linganisha Isaya 29:11, 12.) Kwa kweli, kitabu The Encyclopedia of the Jewish Religion kinasema hivi: “Inaonekana hali ya kujua kusoma na kuandika ilienea kote katika Israeli wa kale.”

Amri za Mungu zilipasa kuandikwa kwenye mihimili ya mlango na kufungwa mikononi​—na ingalikuwa kazi isiyo na maana kufanya hivyo kwa watu ambao hawakuweza kusoma. (Kumbukumbu la Torati 6:8, 9; 27:8) Mfalme alipaswa kuandika nakala yake mwenyewe ya sheria na kuisoma kila siku. (Kumbukumbu la Torati 17:15, 18, 19) Mwanamume mmoja kijana wa Sukothi aliyaandika majina ya wanaume wenye kuongoza watu katika mji wa kwao.​—Waamuzi 8:14.

Wenye kisomo sio peke yao waliojua kusoma na kuandika. Katika maelezo yake juu ya kitabu cha Waamuzi, James D. Martin aliandika akasema kwamba “mengine ya maandishi yenye ushuhuda ulio wa zamani zaidi yanayoonyesha watu walitumia mwandiko wa alfabeti (a, b, c, na kadhalika) yamekwaruzwa kwenye kuta za mapango na watumwa waliokuwa katika mashimo ya madini ya Sinai.” Amosi alikuwa mfuga kondoo wa hali ya chini. Mika alikuwa nabii wa mashambani wa kijiji cha Moreshethi. (Amosi 1:1; Mika 1:1) Hata hivyo wote wawili waliandika vitabu vya Biblia.

Kitabu kisichohesabiwa kuwa kati ya vitabu vinavyokubalika vya Maandiko Matakatifu, Wamakabayo cha Kwanza, ambacho kinaelekea kuwa kiliandikwa karibu na sehemu ya mwisho wa karne ya pili K.W.K., kinaonyesha kwamba watu walikuwa na nakala za ile Torati katika nyumba zao. (1 Wamakabayo 1:55-57) Yosefo mwanahistoria Myahudi aliyataja maoni yake ya karne ya kwanza kwamba ile Torati inaagiza kwamba watoto “watapaswa kufundishwa kusoma, na watajifunza sheria za babu zao hata matendo yao.”​—Kitabu Against Apion, II uku. 375 (25).

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki