Maelezo ya Chini
c “Hisia ya moyo inayojitokea yenyewe [kumwelekea Mungu],” ndivyo Lexicon ya Edward Robinson inavyofafanua neno la awali la Kigiriki eu·seʹbei·a. J. A. H. Tittmann, katika kitabu chake Remarks on the Synonyms of the New Testament, anaongeza hivi: “[Utawa] ni kumwogopa Mungu kunakojionyesha kwa matendo, . . . lakini [kicho] kinaonyesha maelekeo yale, yanayohofu na kuepuka kufanya cho chote kilicho kinyume cha yanayofaa, . . . [utawa] ni nguvu za kumcha Mungu maishani.”