Maelezo ya Chini
b Wazee katika kundi la Kikristo wana daraka la kushughulikia vitendo vya kuvunja sheria ya Kimungu, kama vile wivi, uuaji, na ukosefu wa adili. Lakini Mungu hakuwawekea wazee wa kundi takwa la kufikiliza sheria na amri za Kaisari. Kwa hiyo, Paulo hakujiona akiwa na lazima ya kumpeleka Onesimu mikononi mwa wakuu Waroma. Onesimu alikuwa mtoro chini ya sheria ya Kiroma. (Filemoni 10, 15) Bila shaka, mtu akivunja vibaya sana sheria ya serikali, awe na sifa ya kuwa mvunjaji sheria, yeye hangekuwa mfano mwema na anaweza hata kutengwa na ushirika. (1 Timotheo 3:2, 7, 10) Ikiwa uvunjaji sheria wake ulihusika katika kusababisha kifo cha wengine, anaweza kuwa na hatia ya damu.