Maelezo ya Chini
a Katika nyakati za kisasa, wanahistoria wa Kanisa Katoliki la Kiroma wameshikilia kwamba kugongomewa kwa hoja hizo na Lutheri kwenya mlango wa kanisa lenya ngome katika Wittenberg katika Oktoba 31, 1517 ni “hadithi ya kimapokeo ya makanisa ya Kiprotestanti.” Hata hivyo, uhakika usiofanyiwa ushindani ni kwamba yeye alimwandikia Askofu Mkuu barua ya heshima siku hiyo na akaingiza ndani nakala ya hoja hizo. Lutheri alimwomba awakaripie wahubiri wake wenye kuuzia watu rehema za dhambi na ayafute maagizo ya kufanya hivyo. Barua ile asilia ingali katika Jumba la Hifadhi za Kiserikali Sweden katika Stockholm.