Maelezo ya Chini
a “Hata mageuzo makubwa yaliyofanywa kwa ujasiri mwingi zaidi yaliacha kukiwa bado na wakulima maskini, washarifu wenye mapendeleo makubwa mno wenye kutozwa kodi kidogo tu, tabaka ya watu wa cheo cha katikati wasiohusishwa vya kutosha katika serikali na jamii . . . Lazima isemwe kwamba ingawa utawala wenye mamlaka kamili ulianza kukabiliana na masuala ambayo hayangeweza kupuuzwa tena baada ya huo kuzinduka, haukuweza kuandaa matatuzi halisi ndani ya magumu halisi ya kisiasa na kiuchumi ya enzi hiyo.”—Western Civilization—Its Genesis and Destiny: The Modern Heritage.