Maelezo ya Chini
a The Encyclopedia Americana na Great Soviet Encyclopedia pia zaafikiana kwamba utawala wa Artazakse uliisha katika 424 K.W.K. Ulianza lini? Katika 474 K.W.K. Kwa kuunga mkono hilo, mwandiko mmoja wa kiakiolojia umepewa tarehe katika mwaka wa 50 wa Artazakse; mwingine waonyesha kwamba cheo chake kilichukuliwa na mwandamizi katika mwaka wake wa 51. Tukihesabu kuanzia 424 K.W.K. miaka 50 kamili kurudi nyuma, twaja kwenye tarehe ya 474 K.W.K. kuwa ndio mwanzo wa utawala wake. Kwa hiyo, mwaka wa 20 wa Artazakse, wakati ambapo amri ilitolewa, ungekuwa miaka 19 kamili ndani ya utawala wake, yaani, 455 K.W.K. Kwa maelezo zaidi, ona Insight on the Scriptures, Buku 2, ukurasa 616, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.