Maelezo ya Chini
a Kwa habari ya “ukuu wa jamii ya Kiarya,” The New York Times la Februari 17, 1940, lilinakili mshikilia-cheo mmoja Mkatoliki wa Chuo Kikuu cha Georgetown kuwa akisema kwamba “alikuwa amemsikia Adolf Hitler akisema kwamba ile Milki Takatifu ya Kiroma, iliyokuwa milki ya Kijeremani, ni lazima ianzishwe upya.” Lakini mwanahistoria William L. Shirer anaeleza tokeo: “Milki ya Tatu iliyozaliwa katika Januari 30, 1933, Hitler alijisifu, ingedumu kwa miaka elfu moja, na katika kawaida ya usemi wa Kinazi ilitajwa mara nyingi kuwa ile ‘Milki ya Miaka Elfu Moja.’ Ilidumu kwa miaka kumi na miwili na miezi minne.”