Maelezo ya Chini
a “Watoza kodi walichukiwa na wenyeji Wayahudi wa Palestina hasa kwa sababu nyingi: (1) walikusanya pesa kwa ajili ya mamlaka ya kigeni ambayo ilimiliki bara la Israeli, hivyo kwa njia isiyo wazi, wakiwa wanaunga mkono tendo lao ovu; (2) walikuwa na sifa mbaya ya kuwa na tabia mbaya, wakiendelea kuwa matajiri kwa hasara ya wengine wa watu wao wenyewe; na (3) kazi yao iliwahusisha kwa kawaida na Wasio Wayahudi, ikiwafanya kutokuwa safi kulingana na kanuni za kidini. Dharau kwa watoza kodi inapatikana katika A[gano] J[ipya] na vichapo vya warabi pia . . . Kulingana na hivi vilivyotajwa sasa, chuki ingeenezwa hata kwa familia ya mtoza kodi.”—The International Standard Bible Encyclopedia.