Maelezo ya Chini
a “Katika maana iliyo pana, neno ‘Uasherati’ kama lilivyotumiwa kwenye Mathayo 5:32 na 19:9 kwa wazi linamaanisha namna nyingi za ngono haramu zisizo halali zinazofanywa nje ya ndoa. Neno porneia [neno la Kigiriki linalotumiwa katika maandiko hayo] linatia ndani matumizi ya kiungo (viungo) cha uzazi kwa njia ya ukosefu mkubwa wa adili cha angaa mwanadamu mmoja (yawe ni matumizi ya kiungo hicho kwa njia ya asili au kwa njia iliyopotoshwa); pia, ili lihesabiwe hivyo ni lazima kuwe kulikuwa na mwingine mwenye kuhusika katika huo ukosefu wa adili—mwanadamu, awe ni mwanamume au mwanamke, au mnyama.” (Mnara wa Mlinzi, Januari 1, 1984, kurasa 6, 7) Uzinzi: “Uhusiano wa kingono wa hiari kati ya mtu aliyefunga ndoa na mwenzi mwingineye yote asiye mume au mke halali.”—The American Heritage Dictionary of the English Language.