Maelezo ya Chini
a Nyakati nyingine viongozi wa kidini wenyewe walikuwa wanavita. Katika Mapigano ya Hastings (1066), askofu Mkatoliki Odo alitetea kuhusika kwake sana katika vita kwa kutumia rungu lenye vyuma vinavyochomoza badala ya upanga. Alidai kwamba ikiwa damu haikumwagwa, mtu wa Mungu angeweza kuua kihalali. Karne tano baadaye, Kardinali Ximenes aliongoza binafsi shambulio la Kihispania dhidi ya Afrika Kaskazini.