Maelezo ya Chini
a Hata hivyo, Yehova hafikirii mambo mengine anapoamua kuonyesha msamaha. Madhalani, kama mtenda kosa hajui viwango vya Mungu, hali yake ya kutojua yaweza kupunguza uzito wa hatia. Yesu alipouliza Baba yake awasamehe wauaji wake, yaonekana Yesu alikuwa akizungumza juu ya wanajeshi Waroma, waliomwua. Wao ‘hawakujua watendalo,’ wakikosa kujua yeye alikuwa nani hasa. Hata hivyo, viongozi wa kidini waliosababisha mauaji hayo walikuwa na hatia kubwa zaidi—na kwa wengi wao, msamaha haungewezekana kwao.—Yohana 11:45-53; linganisha Matendo 17:30.