Maelezo ya Chini
a Ingawa Biblia husema kwamba “cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna,” hii haimaanishi kwamba lazima kuteseka kwa mtu kuwe adhabu ya kimungu. (Wagalatia 6:7) Katika ulimwengu huu unaoongozwa na Shetani, mara nyingi waadilifu hukabili matatizo mengi zaidi kuliko waovu. (1 Yohana 5:19) “Mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu,” Yesu akawaambia wanafunzi wake. (Mathayo 10:22) Maradhi na namna nyingine za taabu zaweza kumkumba yeyote wa watumishi waaminifu wa Mungu.—Zaburi 41:3; 73:3-5; Wafilipi 2:25-27.