Maelezo ya Chini
c Hilo ni kosa lililofanywa na madhehebu kadhaa ya Jumuiya ya Wakristo. Lutheri lilikuwa jina ambalo maadui wa Martin Luther walibandika wafuasi wake, ambao nao walilikubali. Vivyo hivyo, Wabaptisti walikubali jina walilokuwa wamebandikwa na watu wa nje kwa sababu walihubiri ubatizo wa kuzamisha. Kwa njia ambayo karibu ifanane na hiyo, Wamethodisti walikubali jina walilobandikwa na mtu wa nje. Kuhusu jinsi Society of Friends ilivyokuja kuitwa Quakers (watetemeshaji), The World Book Encyclopedia chasema hivi: “Neno Quaker awali lilikusudiwa kudhihaki Fox [mwanzilishi], aliyemwambia hakimu mmoja Mwingereza ‘atetemekee Neno la Bwana.’ Hakimu huyo akamwita Fox ‘quaker.’”