Maelezo ya Chini
b Bila shaka, sawa na maneno mengi yawezayo kutumiwa kwa njia nyingi sana, neno neʹphesh pia lina maana mbalimbali. Kwa mfano, yaweza kurejezea mtu wa ndani, hasa katika kurejezea hisia zenye kina. (1 Samweli 18:1) Yaweza kurejezea pia maisha ambayo mtu hufurahia akiwa nafsi.—1 Wafalme 17:21-23.