Maelezo ya Chini
c Baadhi ya nyimbo katika kitabu chetu cha wimbo cha sasa, Mwimbieni Yehova Sifa, zimedumisha ule ulinganifu wa sauti wenye sehemu nne kwa manufaa ya wale wanaofurahia kuimba sehemu za ulinganifu wa sauti. Hata hivyo, nyimbo nyingi zimepangwa ili kuwa na mfuatano wa piano na zilipewa mpangilio wa kimuziki unaojaribu kuhifadhi asili za kimataifa za huo muziki mbalimbali. Kutunga sauti zenye ulinganifu kwa ajili ya nyimbo zilizoandikwa bila ule ulinganifu wa sauti wenye sehemu nne kamili huenda ukaandaa uongezeo wenye kupendeza kwenye kuimba kwetu mikutanoni.