Maelezo ya Chini
a Udonati ulikuwa farakano la “Kikristo” la karne ya nne na ya tano W.K. Wafuasi wake walidai kwamba uhalali wa matendo ya kidini hutegemea sifa za kiadili za mhudumu na kwamba ni lazima kanisa liondoe kutoka kwa washiriki wake watu wenye hatia ya dhambi nzito. Uaria ulikuwa harakati ya “Kikristo” ya karne ya nne ambao ulikana uungu wa Yesu Kristo. Ariasi alifundisha kwamba Mungu hakuzaliwa wala hana mwanzo. Kwa sababu Mwana amezaliwa, hawezi kuwa Mungu katika maana sawa na vile Baba alivyo. Mwana hakuwako tangu umilele wote lakini aliumbwa na huwako kwa mapenzi ya Baba.