Maelezo ya Chini
a Watafiti fulani husisitiza kwamba Yuda ananukuu kutoka katika kichapo cha kubuniwa kiitwacho Book of Enoch. Hata hivyo, R. C. H. Lenski aandika: “Twauliza: ‘Ni nini chanzo cha habari zilizokusanywa kufanyiza kichapo hiki, yaani Book of Enoch?’ Kitabu hiki ni tokeo la habari zilizoongezwa, na hakuna aliye na hakika juu ya tarehe za sehemu zake mbalimbali . . . ; hakuna awezaye kuwa na hakika kwamba baadhi ya maelezo yake labda, hayakutolewa kwa Yuda mwenyewe.”