Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO

Maelezo ya Chini

a Wakristo fulani wanaofanya kazi hospitalini wamelazimika kufikiria jambo hili la mamlaka. Tabibu aweza kuwa na mamlaka ya kutoa agizo mgonjwa apewe dawa fulani au atibiwe kwa kufuata utaratibu fulani. Hata ikiwa mgonjwa hakatai, daktari Mkristo mwenye mamlaka anawezaje kuagiza utiaji-damu mishipani au utoaji-mimba, akijua vile Biblia isemavyo kuhusu mambo hayo? Kinyume cha hilo, huenda muuguzi aliyeajiriwa hospitalini asiwe na mamlaka hiyo. Anapofanya utumishi wake mbalimbali wa kawaida, huenda daktari akamwagiza apime damu kwa kusudi fulani au atunze mgonjwa aliyekuja ili kutoa mimba. Kwa kupatana na kielelezo kilichorekodiwa kwenye 2 Wafalme 5:17-19, huenda akakata kauli kwamba kwa kuwa si yeye mwenye mamlaka ya kuagiza utiaji-damu mishipani au utoaji-mimba ufanywe, basi anaweza kutoa utumishi wa kibinadamu kwa mgonjwa. Bila shaka, bado atalazimika kuifikiria dhamiri yake, ili ‘ajiendeshe mbele ya Mungu kwa dhamiri iliyo safi.’—Matendo 23:1.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki