Maelezo ya Chini
a Idadi kamili ya wanajeshi na raia ambao wamekufa haijulikani vizuri. Kwa mfano, kitabu Facts About the American Wars cha 1998 chasema hivi kuhusu Vita ya Ulimwengu ya Pili pekee: “Habari nyingi zinataja kwamba jumla ya watu waliokufa kwa sababu ya Vita ya Ulimwengu ya Pili (wanajeshi na raia) ni milioni 50 lakini wengi ambao wamechunguza suala hilo vizuri wanaamini kwamba waliokufa ni wengi zaidi—maradufu ya idadi inayotajwa.”