Maelezo ya Chini
a Idara ya Huduma za Habari za Kihospitali husimamia mfumo wa kimataifa wa Halmashauri za Uhusiano na Hospitali mbalimbali. Halmashauri hizo zimefanyizwa na wajitoleaji Wakristo ambao wamezoezwa kuendeleza ushirikiano baina ya madaktari na wagonjwa ambao ni Mashahidi. Kuna Halmashauri za Uhusiano na Hospitali zaidi ya 1,400 ambazo husaidia wagonjwa katika nchi zaidi ya 200.