Maelezo ya Chini
c Nukuu hili la mwisho linalopatikana katika andiko la Matendo 20:35, limenukuliwa na mtume Paulo peke yake, ijapokuwa maana ya maneno hayo imedokezwa katika vitabu vya Injili. Huenda Paulo alipokea maneno hayo kwa mdomo (ama kutoka kwa mwanafunzi fulani aliyemsikia Yesu akisema maneno hayo au kutoka kwa Yesu aliyefufuliwa) au kwa kufunuliwa na Mungu.—Matendo 22:6-15; 1 Wakorintho 15:6, 8.