Maelezo ya Chini
b Inaonekana kwamba masinagogi yalianza kutumiwa wakati wa ile miaka 70 ya utekwa huko Babiloni wakati ambapo hakukuwa na hekalu au muda mfupi baada ya Wayahudi kurudi kutoka utekwani, hekalu lilipokuwa likijengwa upya. Kufikia karne ya kwanza, kila mji wa Palestina ulikuwa na sinagogi lake, miji mikubwa zaidi ilikuwa na masinagogi kadhaa.