Maelezo ya Chini
a Kuhusu urefu wa wakati wa kipindi cha Unadhiri, mtu aliyeweka nadhiri ndiye aliyeamua muda ambao angeendelea kuwa chini ya nadhiri hiyo. Hata hivyo, kulingana na mapokeo ya Wayahudi, mtu hangeweza kuweka nadhiri kwa muda unaopungua siku 30. Ilifikiriwa kwamba kuweka nadhiri kwa muda unaopungua siku 30 kungeifanya ionekane kuwa jambo la kawaida tu.