Maelezo ya Chini
a Huenda maneno hayo yakarejelea kwa njia isiyo ya moja kwa moja kazi za ofisa wa hekalu la mlimani huko Yerusalemu. Wakati wa makesha ya usiku alitembea hekaluni ili kuona ikiwa walinzi Walawi walikuwa macho au walikuwa wamelala mahali pao pa kazi. Mlinzi yeyote aliyepatikana amelala alipigwa kwa kijiti, na huenda mavazi yake ya nje yalichomwa kama adhabu ya kumwaibisha.