Maelezo ya Chini
b Kwa kawaida Mlima Karmeli huwa na mimea mingi ya kijani, kwa sababu pepo zenye mvuke kutoka baharini zinapanda juu ya mabonde yake na hivyo kutokeza mvua na umande kwa ukawaida. Kwa kuwa Baali alionwa kuwa ndiye anayeleta mvua, mlima huo ulikuwa kituo muhimu cha ibada ya Baali. Mlima Karmeli ambao ulikuwa umekauka kwa sababu ya ukame ulikuwa mahali panapofaa zaidi pa kufunua ibada ya Baali kuwa ya udanganyifu.