Maelezo ya Chini
a Hati za Biblia zinazotegemeka zaidi hazina mistari ya 44 na 46. Wasomi wanasema kwamba huenda mistari hiyo miwili iliongezwa baadaye. Profesa Archibald T. Robertson anaandika hivi: “Mistari hiyo miwili haipatikani katika hati bora zaidi na za kale zaidi. Ilitokana na vikundi vya hati za Magharibi na Siria (Bizantiamu). Mistari hiyo inarudia tu mstari wa 48. Kwa hiyo, tunaondoa mistari ya 44 na 46 ambayo si sahihi.”