Maelezo ya Chini
a Ulafi ni mtazamo wa akili, na mlafi anakula kupita kiasi au kwa pupa. Kwa hiyo, ulafi hauonekani kupitia ukubwa wa mwili wa mtu, bali kupitia mtazamo wake kuhusu chakula. Mtu anaweza kuwa na unene wa kadiri au hata awe mwembamba lakini bado awe mlafi. Kwa upande mwingine, mtu anaweza kuwa mzito kupita kiasi kwa sababu ya ugonjwa au anaweza kurithi hali ya kuwa mnene kupita kiasi. Jambo kuu ni ikiwa mtu, hata awe mzito kadiri gani, anakula kwa pupa nyingi sana.—Ona “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” katika gazeti la Mnara wa Mlinzi la Novemba 1, 2004.