Maelezo ya Chini
a Ni muhimu kujua kwamba Yona alitoka Galilaya kwa sababu Mafarisayo walisema hivi kwa kiburi kumhusu Yesu: “Chunguza uone kwamba hakuna nabii atakayeinuliwa kutoka Galilaya.” (Yohana 7:52) Watafsiri na wachunguzi wengi wamedokeza kwamba Mafarisayo walikuwa wakizungumza kwa ujumla kwamba hakuna nabii aliyewahi au atakayewahi kutoka mji wa hali ya chini wa Galilaya. Ikiwa ndivyo, walipuuza historia na pia unabii.—Isaya 9:1, 2.