Maelezo ya Chini
a Inasemekana kwamba homa ya Kihispania iliambukiza kati ya asilimia 20 na asilimia 50 ya watu wote ulimwenguni wakati huo. Huenda virusi vya ugonjwa huo vilisababisha vifo vya kati ya asilimia 1 na asilimia 10 ya watu walioambukizwa virusi hivyo. Kinyume chake, virusi vya Ebola haviwaambukizi watu kwa ukawaida, lakini katika visa fulani vimesababisha vifo vya asilimia 90 hivi ya watu walioambukizwa.